“Tulianza kutana mwezi januari mwaka huu ili kuomba shirika Regideso mafasirio, kwa kuwa raia wanalipa pesa kuhusu maji ambayo hawapate. Tuliona muhimu kuarifu viongozi na kuhamasisha raia ili pamoja kutafuta suluhu kwa swala hili. Tumeanza kazi hiyo katani Panzi ambako viongozi husika walikutana na raia na leo tunapatikana mtaani Kadutu. Tuliongea na raia mbele ya kiongozi wa Regideso, na mbele ya mjumbe wa idara ya nishati, viongozi wa kata na wale chembe chembe”, anena Byamungu Kazimire Samuel.
Huyu aongeza kwamba raia walieleza shida zinazo wakumba kuhusu ukosefu wa maji. Ilionekana kwamba jukumu ni kwa pande zote husika kutokana na mafasirio ya raia.
Kuna watu wenyi kujenga juu ya vyombo vya Regideso na wengine wasiotaka kulipa maji. Kwake kiongozi kiufundi kwenyi shirika hilo Salumu Mwamba, shida ya maji mtaani Kadutu itatatuliwa. Shirika Regideso litatengeneza vyombo vyake humo, na kila mkaazi atapata maji kabla ya miezi tatu>> anena mwana harakati huu wa shirika la raia baada ya kikao.
Huyu anena kwamba juma mosi ijayo ni zamu ya mtaa wa Bagira. Na baadae kutowa ripoti kwa ngazi za juu mjini Kinshasa. Akiamini kwamba suluhisho litapatikana toka ngazi za juu. Na kuomba raia kutumika bega kwa bega ili kufikia lengo.