Hayo yalifahamishwa naye Injinia Didier Lwisa mbele ya viongozi wa mahali na kwa raia wa Goma kwa jumla. Huu ni mradi ukitekelezwa na shirika SGC nchini DRC.
Kazi za mradi ambazo zingianza mwezi septemba, zilianza mwezi januari 2024 kutokana na shida ndogo ndogo.
Tunaamini kwamba mwisho mwezi disemba 2024 kazi zitakoma na mwezi januari kazi zitaweza kuanza ndani ya jumba anena mhusika na ujenzi.
Ila wamoja husema kwamba hawakushirikishwa kwa kazi za mradi. Mfano wake Rocky Ngelema Tchomba ambaye ni prezidenti wa Muungano wa walemavu kwa jina Tuungane. Huyu aomba viongozi nawo kuwashirikisha.
<< Ijapo tunashukuru viongozi kwa kazi hizo, Ila twaona kwamba watu walemavu nawo hawashirikishwe ndani ya mradi. Ingelikuwa heri nasi tushirikishwe kulingana na hali yetu,>> anena Rocky Ngelema.
Tufahamishe kwamba kazi za ujenzi wa jumba kwenyi mpaka mdogo Rwanda DRC zasonga mbele ijapo matatizo. Mpaka huo ni wa lazima kwa kuwa unarahisisha kazi za byashara kati ya nchi mbili. Pamoja na hayo unaweka mkazo kiusalama kwa nchi hizo mbili na kuinua maendeleo kiuchumi kwenyi kanda la maziwa makuu. Milioni 7 dola za marekani ndizo zitatumiwa kwa kukomesha kazi. Na wafanya kazi mia 3 ndio wanachapa kazi.