Kamisa mkuu Kapend Kamand Faustin pia mea wa mji anena kwamba jambazi umoja alinaswa usiku wa tarehe 14 kuamkia tarehe 15 Juni wakiiba huko Irambo katani Mapendo. Aina ya pili ni wevi ni walio naswa kwenyi kata la Katoyi wakitumia silaha. Aina ya tatu ni wenyi kujiita Wazalendo ijapokua ni uongo mtupu. Hawa walianguka ndani ya mtego wilayani Nyiragongo wakitumia silaha na wakiwa na vitambulisho vya polisi. Aina ya nne ni waendesha piki piki wakipeleka bangi kwenyi Kambi ya wahamiaji ya Bulengo, afasiria Meja José, mhusika operesheni mjini Goma.
Mea wa mji kamisa mkuu Kapend Kamand ashukuru kwa uhusiano na ushirika kila leo ndani ya mji. Akisisitiza raia wote washiriki kwa kusaka amani mjini Goma. Akiwaomba kuwa macho ili kuwepo nguvu yakujuwa adui asije akaharibu mji. <<Adui ana lengo la kutumikisha vileo ili raia wapate kuinuka dhidi ya viongozi,>> anena. Akiomba waviepuke kwani ni moja wapo ya chanzo cha kukwamisha usalama mjini.