Wandishi wahabari walikumbushwa kazi yao katika lengo la kuishi pamoja kijamii. Baadae walifunzwa kuhusu kutafuta habari kwa kutumia akili inayotengenezwa na binaadam ambayo inatwa Intelligence Artificielle katika lugha la kimombo. Technolojia hiyo nyipya itasaidia wapasha habari kufanya haraka kazi yao na kuisahisha.
Prezidenti wa shirika la wandishi habari Kivu ya Kaskazini Rosalie Zawadi aomba wandishi habari kuwa makini muda wa kikao. Humo watatowa ujuzi itakayo wasaidia kwa kazi yao ya kila leo. Hasa jimboni humo yenyi kukumbwa na mizozo ya kila aina.
Upande wake mjumbe wa liwali wa jimbo Bi Prisca Kamala ashukuru waandalizi wa icho kikao, akiomba wandishi wahabari kutega sikio wapate kuelewa mengi. Akiongeza mafunzo yatasaidia wapasha habari kutowa habari kamili kwa manufaa ya wote. Muda ambao DRC yashambuliwa na Rwanda . Na kwamba raisi wa taifa ajitahidi kuboresha sekta ya upashaji habari.
Tufahamishe kwamba kazi hiyo itadumu muda wa siku tatu.