Vyanzo hivyohivyo vinazungumzia majaribio ya jeshi la Kongo kurejesha udhibiti wa maeneo haya yaliyokaliwa kwa miezi kadhaa na waasi.
Jeshi lilishambulia Jumatano, Mei 15, kutoka eneo la uvuvi la Vitshumbi.
Kulingana na vyanzo vya ndani, jeshi limeazimia kuwatimua waasi wanaojaribu kupinga.
Kwa mujibu wa Radio Okapi ambayo inatupa taarifa hizi, nguvu ya ufyatuaji huo imepungua tangu saa 10 alfajiri kwa saa za Rwindi na Kibirizi, huku utulivu ukionekana Vitshumbi Alhamisi hii, vyanzo vyetu vinabainisha.
Zaidi ya hayo, hali ya utulivu imerejea Alhamisi hii katika kijiji cha Kihondo, karibu na Nyanzale, bado huko Bwito, baada ya kuvamiwa kwa muda mfupi Jumatano jioni na kundi la wapiganaji wa eneo hilo.
Katika eneo jirani la Masisi, ni kijiji cha Kashuga, karibu na Mweso ambacho kilikuwa, mapema Alhamisi hii, shabaha nyingine ya wapiganaji kutoka kundi la NDC-Rénové de Guidon dhidi ya M23. Uvamizi huu ulisababisha, kati ya saa 6 asubuhi na saa 7 mchana kwa saa za huko, harakati za wakazi fulani kuelekea Mweso na Kalembe, vyanzo vya ndani vinaonyesha.