Sherehe za kuandaa mazishi zafanyika mbele ya uwanja wa kandanda de l’unité mjini Goma, wakiweko viongozi wa serkali, wakijeshi na wa kiraia.
Wazuri wa taifa husika na haki ya binaadam Albert Fabrice PUELA alikwenda kujionea nafasi miili zitazikwa, baada ya kupunguza nafasi ambako raia hawa walipoteza maisha kwa kutupiwa bomu.
Waziri huyu anena kwamba kaburi thelasini na tano zimetayarishwa ili kupokea miili ya wahanga wa mauaji toka nchi ya Rwanda kupitia waasi M23.
Waziri husika na haki ya binaadam Albert PUELA anena kwamba nchi ya Rwanda kupitia waasi hawo imefanya mauaji ya kimbari. Na kwamba sherti Umoja wa kimataifa kujihusisha na swala hilo, hâta kama Rwanda haikuweza kusahini makubaliano ya Roma.
Tufahamishe kwamba mawaziri na wanabunge wa taifa toka mjini Kinshasa wanashiriki kwenyi sherehe hiyo ya kuomboleza.