Kivu Kusini: Kisa kipya cha mauwaji charipotiwa katika Kijiji cha Mulima Tarafani Fizi
Kwa mujibu wa vyanzo vya asasi za kiraia (société civile) eneo la Fizi vili wasiliana na kivuavenir.com, Alhamisi hii, Januari 2, 2024, vinasema kuwa askari polisi alimpiga risasi mtu mmoja huko Milima, kijiji kilichopo katika kikundi cha Basilocha, sekta ya Tanganyika katika eneo la Fizi.
Kivu Kusini, usiku wa Jumatano hadi Alhamisi Januari 2, 2024. Sami Bin AmimuCorticoles, makamu wa Rais wa vikosi vya mashirika ya kiraia katika eneo la Fizi, anathibitisha habari hii huku akisisitiza kwamba mwanamume aitwaye Philémon mwenye umri wa zaidi ya miaka 36 aliuawa kwa kupigwa risasi huko Mulima mida ya samoja ya usiku na afisa wa polisi wakati idadi ya watu walikuwa wakisherekea sherehe ya Mwaka mpya 2025. Mwathiriwa alikuwa akipigana na raia wengine kama ilivyozoeleka siku zote wakati wa tafrija (furaha) mtu anapokuwa amelewa hivyo polisi hufika na kumfyatulia risasi mtu.
Afisa huyo wa polisi muuaji alitoweka hewani baada ya mkasa huo na mpaka sasa hakujulikana alikoelekea.
Kufuatia hali hiyo, asasi za kiraia zinalaani vikali kitendo hicho cha kudharauliwa na kutoa wito kwa haki kufanya kazi yake ili kuweka wazi sababu za mauaji haya.