Lengo la mkutano huo, Umoja wa Ulaya uilitaka kujuwa moja kwa moja kuhusu hali ya kibinadamu mashariki mwa nchi, haswa katika Kivu Kaskazini.
“Nilikuja nchini hapa kongo ilinipate kukuelezea mshikamano wangu na uungaji mkono wa EU kwa watu wa Kongo, haswa wale wanaoteseka mashariki mwa nchi,” Janez Lenarčič akizungumza baada ya mkutano na Rais Tshisekedi.
Alisisitiza kuendelea kujitolea kwa Umoja wa Ulaya kutoa msaada wa dharura wa kibinadamu kwa watu walio patwa namagumu ya vita na migogoro katika eneo hilo.
Baada ya ziara hii, Mujumbe huyo atatembelea kambi kadhaa za watu waliokimbia makazi yao katika jimbo hilo Jumanne hii, ikiwa ni pamoja na ile ya Mugunga ambayo hivi majuzi ilikumbwa na milipuko ya silaha nzito asema Umoja wa Ulaya