Kwa muda mrefu, katiba hiyo hiyo ilisemekana kwamba ikiwa Rais Tshisekedi atakuwa na wengi, kila kitu kitafanya kazi kama kawaida. Leo Rais anasema ni Katiba inayozuia uwanzishwaji wa Serikali. Ni makosa. Tatizo liko kwingine.
Rais Kabila aliiongoza nchi hii kwa miaka 18 kwa katiba hiyo hiyo. Aliweka serikali na kuzifanyia mabadiliko kama alivyotarajia bila tatizo lolote. Ikiwa Rais hajui jinsi ya kuifanya nchi ifanye kazi kwa katiba ile ile, tatizo ni yeye mwenyewe.”