Matokeo yakipelekwa kwenyi mahakama kuu za mji wa Kinshasa pa Gombe na Matete.
Ni wafanya kazi yapata 961 ndio wapokonya pesa ya serkali kiholela, wakipokea kwenyi widhara mbali mbali nchini DRC.
Miongoni mwao, wamoja wapokea mishahara pasipo kufanya kazi, wengine wapokea mishahara mbili, tatu na kadhalika.
Ripoti iliyotangazwa inaeleza namna hîi:
145. 604 ni wafanya kazi wenyi kupokea mishahara wakiwa na kitambulisho bandia walicho kitengeneza ili ya kupokea mishahara.
53.328 wafanya kazi ni wenyi zaidi ya kitambulisho moja kwenyi orodha, wakipokea kupitia jina moja.
93. 356 wafanya kazi wenyi kuwa na kitambulisho moja na wafanya kazi wengine.
43. 725 wafanya kazi wenyi kulipwa bila jina zao kwenyi daftari ya orodha kutoka nafasi watumika na kadhalika.
Huo si mshangao zaidi, wakongomani hawa pendi inch nyawo!