Ni katika lengo la kutaka kutekeleza amani, maendeleo ya kudumu, kurejesha usalama wilayani humo.
Washiriki kikao walisema kukerwa na hali ya usalama makwao, yaani uporaji usiku na mchana, mauaji ya raia na kadhalika.
Prezidenti wa Kabila la wakumu Jean Claude Bahati aomba viongozi kujihusisha kinaganaga na usalama ili kukinga raia vilivyo
<<Baada ya kikao administreta ahakikisha kwamba mbinu zitachukuliwa ili kutekeleza usalama wilayani Nyiragongo , ambayo ni mhanga wa mauaji na wizi anena Jean Claude Bahati.
Kuhusu uchaguzi wa kamati ya Kabila la wakumu Jean Claude aomba eneo zote za usultani wa Bakumu zishirikishwe ndani ya kamati nyipya. Akisema kwamba uchaguzi ni hapa karibuni. Kwa kuwa kamati ya mseto inafanya kazi ili kufikia kutayarisha uchaguzi na kufikia kamati kamili.
Administreta aliahidi kusindikiza kiusalama kazi hizo.
Mwishowe washiriki kikao waliomba raia kutotega sikio adui, muda ambao Nyiragongo yakumbwa na usalama mdogo ikisababishwa na waasi wa M23.